
Baadhi ya mahakama, shule na vituo vya treni vimelazimika kufungwa kutokana na kutolewa kwa onyo la bomu nchini Urusi.
Kulingana na kituo cha habari cha Rushia, shule 19, mahakama 7 na vituo vya treni 6 vimetolewa onyo la uwezekano wa mlipuko wa bomu.
Wanafunzi, wafanyakazi na wageni wa maeneo hayo walilazimika kuhamishwa baada ya tangazo hilo.
Polisi wanaendelea kufanya msako katika maeneo husika.