TAMWA Pemba yatahadharisha Mpeta na Udhalilishaji.

Imeandikwa na Salmin Juma- Pemba

Email:salminjsalmin@gmail.com

Mratibu wa Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania upande wa Zanzibar kisiwani Pemba, Bi Fat hiya Mussa Said ametoa wito kwa wazazi na walezi wa watoto kisiwani humo kuwa makini sana na watoto wao wasije kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji vinavyoendelea kutokea siku hadi siku kisiwani humo kwani athari ya vitendo hivyo ni kubwa ambayo itamugharibu siku nyingi mtoto hadi kukaa sawa.

Wito huo ameutoa jana alipokua akizungumza na mwandishi wa habari hizi juu ya uchumwaji  wa zao la karafuu kisiwani humo hivi sasa ambapo inaelezwa kuwa, baadhi ya vitendo vya udhalilishaji vimeshawahi kuripotiwa wakati watoto wanapokwenda kuokota mpeta (ni wanao okotoa karafuu zinazo anguka chin).

“hivi sasa ni wakati wa karafuu, mpeta umeshamiri , matukio mbalimbali yanaweza kutokea, wazazi wanatakiwa wawe makini” alisema Mratibu huyo.

Alisema, wazazi wanapaswa kujua watoto wao wanakwenda kuokota mpeta wapi na watakua na nani.

Kwa upande wake mratibu wa wanawake shehia ya Wete Bi Awena Salum Kombo aliwataka wazazi wasikubali kuwa mbali na watoto wao kwani vitendo vya udhalilishaji vimekithiri hivi sasa.

Waonee huruma watoto, wanahitaji kutimiza ndoto zao, usiwarudishe nyuma kwa kuwadhalilishaji, kuwa raia mwema kwao.

Alisema, juzi tu katika kijiji cha Munduli Wete kuna kijana anatuhumiwa kuwabaka watoto wawili kwa pamoja wakati wa usiku walipokua wakirudi kutizama tv mbali na  nyumba .

“aliwavizia, kisha akawabaka, watoto wadogo sana wanasoma nasari” alisema Bi Awena.

Mwananchi mmoja ambae hakupenda jina lake lichapishwe mtandaoni alisema, juhudi zinazofanywa na wadau zinaonekana, hasa TAMWA, akisema wanajitahidi sana kutoa mafunzo lakini bado vitendo hivyo vinaendelea kutokea kila siku” kwani jamani tatizo nini mbona hawa TAMWA kila siku tunawasikia wanatoa elimu lakini vinatokea, nachoka asa, sijui nini”

Aliwaomba wazazi kwa kusema, hali jinsi ilivyo  hakuna wa kumuamini kwa mtoto, ikiwa mpaka wazazi wa kiume washasikika kuwabaka watoto wo, hivyo ni lazima wanawake kuhakikisha watoto wao wanakua katika macho yao kila wakati.

chanzo:mtandao wa pembatoday